KOCHA wa timu ya Taifa ya Uingereza Fabio Capello amesema atabwaga manyanga kuinoa timu hiyo baada ya michuano ya Kombe la Ulaya (Euro 2012).
Baada ya kufanya vibaya katika Kombe la Dunia wadau wengi walikuwa wakitaka kocha huyo ajiuzulu, lakini Muitaliano aliweza kuwaziba midomo baada ya kuingoza vyema timu hiyo kwa kushinda mechi mbili za kutafuta tiketi ya michuano ya Ulaya dhidi ya Bulgaria na Switzerland.
Wakiwa na pointi sita na magoli katika mechi hizo mbili, timu hiyo inaonekana iko katika nafasi nzuri ya kufuzu michuano hiyo na kama wakishinda mchezo wao dhidi ya Montenegro mwezi ujao basi watakuwa wamejihakikishia nafasi hiyo.
Hata hivyo, inavyoonekana kama Uingereza itaendelea kucheza katika kiwango kizuri kama hicho na kufuzu kucheza michuano hiyo, itakuwa ni kazi ya mwisho ya Capello kama Kocha.
Wakati akiulizwa kuhusu michuano hiyo kama itakuwa ndio ya mwisho kwake kufundisha timu hiyo alijibu kwa ufupi "Ndio."
"Tunatakiwa kufuzu kwanza lakini baada ya hapo nitakuwa mzee zaidi." "Nahitaji kufurahia maisha yangu ya uzeeni." alimalizia Capello.
No comments:
Post a Comment