Monday, February 28, 2011

ARSENAL YAENDELEZA UKAME WA VIKOMBE KWA KUKUBALI KIPIGO CHA 2-1 NA BIRMIGHAM KATIKA FAINALI YA CARLING CUP.

Wachezaji wa Arsenal wakijaribu kuokoa bila mafanikio mpira uliopigwa na Nikola Zidic wa Birmigham na kuiandikia timu yake hiyo bao la kwanza katika fainali ya Carling Cup iliyochezwa katika Uwanja wa Wembley.

Mshambuliaji wa Arsenal Robin van Persie akishangilia sambamba na Samir Nasri na Jack Wilshere  mara baada ya  mchezaji huyo kuisawazishia bao katika mchezo huo.

Wachezaji wa Arsenal wakiwa wamejiinamia huku wakiwa hawana kufanya baada ya mshambuliaji wa Birmigham Obafemi Martins kuifungia timu ya bao la pili dakika ya 89 baada ya kutumia makosa yaliyofanywa na kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny na beki wa kati Laurent Koscielny na kuifanya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Maelfu ya watu wakimiminika katika Uwanja wa Wembley kushuhudia mchezo wa huo wa fainali kati ya Arsenal na Birmigham.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger akizungumza na kipa wake Szczesny mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.  

Wachezaji wa Arsenal wakishuka mara baada ya kuchukua zawadi zao za ushindi wa pili katika michuano hiyo. 

Wachezaji wa birmigham wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa Kombe la Carling.

No comments:

Post a Comment