Friday, March 11, 2011

"SING'ATUKI NG'O." MAGATH.

HAMBURG, Ujerumani
KOCHA wa klabu ya Schalke 04 ya nchini Ujerumani Wolfgang-Felix Magath amekanusha taarifa za kuwa mbioni kuachana na klabu hiyo utakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Magath amekanusha taarifa hizo saa chache mara baada ya mchezo wa usiku wa kuakia hii leo kumalizika huko Veltins-Arena ambapo alisema ameshangazwa na taarifa hizo ambazo zilichapishwa kwenye gazeti la Westdeutsche Allgemeine Zeitung la nchini ujerumani hapo jana.

Alisema hafikirii kufanya hivyo na wala hakuna mazungumzo aliyoyafanya na viongozi wa klabu ya Schalke 04 juu ya kuvunjwa kwa mkartaba wake hivyo ataendelea kuwepo hadi mwaka 2013 kama makubaliano yake na viongozi wa ngazi za juu yanavyoelekeza.

Taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la Westdeutsche Allgemeine Zeitung zilieleza kwamba meneja huyo toka nchini Ujerumani anatarajia kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu kufuatia kushindwa kufikia malengo aliyowekewa na uongozi wa klabu yake ya kuhakikisha wanafanya vyema msimu huu na kurejea tena katika ngazi za juu ambazo zitawawezesha kucheza michuano ya barani ulaya.

Malengo hayo yameonekana kumshinda meneja huyo mwenye umri wa miaka 57 kufuatia kikosi chake kuvurunda katika michezo ya ligi hali ambayo imeifanya klabu hiyo kushika nafasi ya kumi ambayo ni ngumu kwa kucheza michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment