Monday, November 1, 2010

TWIGA STARS YAANZA VIBAYA HUKO SAUZI.

JOHANESBURG, Afrika Kusini.
TIMU ya Taifa ya wanawake Twiga Stars jana imeanza vibaya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake kwa kukubali kipigo cha mabao 2-1 timu ya Taifa ya Afrika Kusini 'Banyana Banyana' katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Sinaba, Afrika Kusini.

Wenyeji ndio walikuwa wa kwanza kujipatia bao katika dakika ya 35 ambapo mshambuliaji wake Mamphasha Popela.

Bao hilo liliongeza kasi ya Twiga ambapo dakika ya 43 juhudi zao zilizaa matunda ambapo mshambuliaji machachari wa timu hiyo Easter Chabruma alisawazisha bao hilo na kufanya timu hiyo kwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu.

Bao la pili la Afrika Kusini lilifungwa na mchezaji kiungo Makhabane kwa njia ya penati dakika ya 86.

No comments:

Post a Comment