DAR ES SALAAM, Tanzania
KUTOKANA na muitikio mdogo wa mashabiki wa soka waliojitokeza kushuhudia mchezo wakirafiki baina ya Yanga ya Dar es Salaam na Atletico Paranaense ya Brazil kwenye Uwanja wa Taifa jana ambapo Yanga iligaragazwa kwa mabao 3-2, Rais wa Kampuni ya RPB Oil, Rahma Al Kharoous, amesema kuwa mchezo wa kesho jioni kati ya Simba na timu hiyo kiingilio itakuwa ni bure.
Akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Rahma, ambaye ndiye mratibu wa michezo hiyo ya kirafiki, alisema kuwa ameamua kufanya kiingilio kuwa bure ili mashabiki wengi waweze kujitokeza kushuhudia mchezo huo na kuishangilia timu ya Simba ili kuwapa morari waweze kushinda.
Aidha alisema kuwa iwapo Simba itaweza kuibuka na ushindi basi ataigharamia timu hiyo ya Simba kuisafirisha hadi nchini Brazil kwa ajili ya mchezo wa marudiano na kuwataka mashabiki wengi kujitokeza kushuhudia mchezo huo.
No comments:
Post a Comment