Wednesday, January 19, 2011

JERMAINE JONES ATUA KWA MKOPO BLACKBURN

LONDON, England
KLABU ya Blackburn ya Uingereza imemsajili kiungo Jermaine Jones kwa mkopo katika mkataba wa miezi sita kutoka klabu ya Schalke 04 inayoshiriki ligi ya Bundesliga.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Marekani mwenye umri wa miaka 29 ameungana na mshambuliaji Roque Santa Cruz baada ya dirisha dogo la usajili la Januari kufunguliwa Ewood park.

Bosi wa klabu ya Blackburn Steve Kean amesema usajili huo ni wa manufaa kwa klabu hiyo, na kwa yeyote anayemfahamu Jones atakubali kuwa ni mchezaji mwenye kujituma.

No comments:

Post a Comment