Monday, March 14, 2011

"RUBBEN HAUZWI NG'O." MKURUGENZI.

MUNICH, Ujerumani
KUNA minong'ono iliyozagaa kuwa nyota wa Bayern Munich Arjen Rubben anajiandaa kuhamia Milan mwishoni mwa msimu, Lakini Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Christian Nerlinger ameweka wazi kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka Uholanzi hauzwi ng'o.

"Najisikia kucheka nikisikia minong'ono kama hiyo. Haihitaji ufafanuzi wowote kwa kuwa Arjen hauzwi kwa bei yoyote ile," alisema Nerlinger. "Hakuna ukweli wowote kuhusu uvumi huo."

Nerlinger alisema winga huyo ni muhimili muhimu kwa timu hiyo, akitolea mfano kiwango bora alichokionyesha katika mchezo dhidi ya Humburg wiki iliyopita ambapo Bayern ilishinda mabao 6-0 huku Rubben akipiga mabao matatu.

"Kila mtu ameona katika mchezo wa Jumamosi jinsi gani Arjen alivyo muhimu kwa timu hii."

No comments:

Post a Comment