BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) hii limetoa taarifa rasmi ya kuyahamisha mashindano ya Kombe la Kagame kutoka Zanzibar kama ilivyotangazwa mara ya kwanza na kuyapeleka Sudan.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye imesema mashindano hayo wameamua kuyapeleka Sudan baada ya Zanzibar kushindwa kukidhi vigezo vya kuandaa huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni mapungufu ya fedha.
Alisema baada ya kufanya mabadiliklo hayo ratiba na makundi ya michuano hiyo itapangwa mjini Khartoum, Sudan Jumanne Aprili 12 kabla ya kuanza rasmi kwa michuano hiyo June 21 hadi July 5 mwaka huu.
Alisema kubwa lililopelekea kuyahamisha mashindano hayo kutoka visiwani Zanzibar nchini Tanzania hadi nchini Sudan ni ushawishi uliotolewa na viongozi wa chama cha soka nchini humo ambao wamekubali kuubeba mzigo huo sambamba na kusaka wafadhili.
No comments:
Post a Comment