![]() |
Kutoka kushoto Victor Valdes, Xavi na Erick Abidal wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa Kombe la Klabu Bingwa ya Ulaya usiku huu katika Uwanja wa Wembley, Uingereza. |
![]() |
Wachezaji wa Barcelona wakishangilia bao lao la kwanza dhidi ya Manchester United. |
![]() |
Mshambuliaji wa Barcelona David Villa akipigilia msumari wa mwisho katika jeneza la Man United bao ambalo lilizamisha ndoto za timu hiyo kunyakua ubingwa huo. |
![]() |
Mshambualiaji Leonel Messi akipiga shuti kali ambalo lilimshinda golikipa wa Man United Edwin Van de Sar na kutinga wavuni kuandika bao la pili la timu hiyo. |
![]() |
Messi akishangilia bao lake huku mabeki wa Man United wakiwa wamepigwa na butwaa. |
![]() |
Mshambualiaji wa Man United Wayne Rooney akifunga bao la kufutia machozi. |
![]() |
Van de Sar akiangalia mpira ukitumbukia nyavuni. |
![]() |
Mshambuliaji wa Man United Chicharito ambaye hakung'aa usiku wa leo akipambana na Valdes katika moja ya heka heka za mchezo huo. |
![]() |
Kocha wa Manchester United akiwapongeza wachezaji wa Barcelona kwa ushindi wao. |
![]() |
Nyota wa mchezo Xavi akiwa katika moja ya heka heka ambazo zilizaa bao la kwanza katika mchezo huo. |
![]() |
Rooney na Ryan Giggs wakiwa hawaamini kulipoteza kombe hilo kwa mara ya pili kwa Barcelona tena wakiwa nyumbani, mara nyingine ilikuwa ni fainali za mwaka 2009 zilizofanyika Rome, Italia. |
No comments:
Post a Comment