Katika mechi za ufunguzi hii leo kwenye kituo cha Kilimanjaro timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 ‘Vijana Stars’ itacheza na Kilimanjaro mchana wakati jioni timu ya Arusha itavaana na timu ya Tanga.
Katika kituo cha Tabora kutakuwa na mechi kati ya Mabingwa Watetezi timu ya Singida watakaocheza na timu ya Dodoma, huku mechi nyingine katika kituo hicho ikiwa ni kati ya timu za Kigoma na Tabora zitakazovaana katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Huko Morogoro wenyeji Morogoro wataanza kutupa karata yao kwa kucheza na vijana wa Ilala katika mechi itakayochezwa saa nane mchana kwenye Uwanja wa Jamhuri kabla ya Pwani kuumana na Manyara.
Mechi nyingine za ufunguzi katika kituo cha Mbeya itazikutanisha timu za Mbeya na Iringa katika Uwanja wa Sokoine na mechi ya jioni itakuwa baina ya Rukwa na Temeke.
Mkoani Mtwara wenyeji Mtwara watafungua dimba na Kinondoni katika mechi ya kwanza na baadaye kufuatiwa na mechi kati ya Lindi na Ruvuma.
Na mjini ‘Rock City’ Mwanza mechi za ufunguzi zitawakutanisha timu za Kagera na Mwanza zitakazoshuka dimbani katika uwanja wa soka wa CCM Kirumba.
No comments:
Post a Comment