KLABU ya soka ya Chelsea imemteua rasmi Andre Villa-Boas kutoka nchini Ureno kuwa kocha wa klabu hiyo ambapo anakuwa kocha wa saba katika kipindi cha miaka nane toka bilionea wa Urusi Roman Abramovich aanze kuimiliki klabu hiyo.
Villa-Boas (33), ambaye anafananishwa kocha wa zamani wa klabu hiyo Jose Mourinho ambao wote wanatoka nchi moja, ametia saini ya miaka mitatu jijini London leo baada ya kujiengua katika nafasi ya ukocha katika klabu ya Porto.
Mkataba wa kocha huyo na Porto ulisitishwa Jumanne baada ya Chelsea kuilipa klabu hiyo dola milioni 21.5 ili kumchoa kocha huyo.
Villa- Boas amechukua nafasi ya Carlo Ancelotti baada ya kutimuliwa katika dakika za mwisho msimu uliopita pamoja na kushinda vikombe viwili vya Ligi Kuu na Kombe la Ligi msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment