Wednesday, June 1, 2011

FA YAISHAURI FIFA KUAHIRISHA UCHAGUZI.

LONDON, Uingereza
CHAMA cha Soka nchnini Uingereza (FA) kimelitaka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuahirisha Uchaguzi Mkuu wa Rais uliopangwa kufanyika kesho huko mjini Zurich nchini Uswiz huku Rais wa sasa wa shirikisho hilo Sepp Blatter akisalia pekee yake katika kinyang’nyiro hicho kufuatia mpinzani wake kutoka nchini Qatar Mohamed bin Hammam kujiondoa mwishoni mwa juma lililopita.

Ombi la chama cha soka nchini Uingereza limewasilishwa huko FIFA na mwenyekiti wa chama hicho Daudi Bernstein ambapo amedai kwamba hakuna namna ya kuendelea na uchaguzi huo huku harufu ya rushwa ikishamiri miongoni mwa wajumbe wa kamati kuu.

Pia ombi hilo la FA limeitaka FIFA kuunda kamati huru ambayo itafanya kazi kwa uwazi kwa kusudio la kufunua maovu ambayo yamekua yakifanyika nyuma ya pazia na mwisho kujitokeza hadharani kwa aibu.

Hata hivyo tayari katibu mkuu wa FIFA Jorome Valke ameshatangaza mbele ya waandishi wa habari hatua za kuendelea kwa uchaguzi kama zilizopangwa siku za nyuma kufuatia mgombea Blatter aliesalia ulingoni kusafishwa na kamati ya maadili ambayo ilimfanyia mahojiano mwishoni mwa juma lililopita sambamba na Mohamed Bin Hammam pamoja na Jack Warner.

No comments:

Post a Comment