BRASILIA, Brazil
MCHEZAJI nguli kutoka Brazil Pele amesisitiza kuwa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi lazima afunge mabao 1283 katika kipindi cha uchezaji soka ili aweze kutawadhwa kuwa mchezaji bora aliyewahi pata kutokea.
Akiongea mara baada ya klabu yake ya zamani ya Santos kuifunga Penarol mabao 2-1 kunywakuwa ubingwa wa Amerika Kusini "Copa Libertadores" Jumatano, Pele (70) aliwaambia waandishi wa habari: " Messi bora kuliko Pele? ili amfikie anahitajika kufunga zaidi ya mabao 1283."
Pele ameonekana kujibu mashambulizi ya kocha wa zamani wa Argentina Diego Maradona ambaye alidai Neymar hana kauli nzuri kama ilivyo kwa Pele, baada ya mshambuliaji huyo wa Santos kudai kuwa atakuwa bora zaidi ya Messi kama akibakia Brazil kuliko kwenda kucheza soka Ulaya ambapo Real Madrid imeonekana kumuhitaji mchezaji huyo.
"Neymar ana kipaji kikubwa. Ni mategemeo yangu Neymar hatakuwa kama Messi, ambaye anacheza vizuri katika klabu yake lakini hafanyi lolote kwa nchi yake [Argentina]." alisema Pele.
Messi amefunga mabao 31 katika Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), na mabao 12 katika Champions League likiwemo moja katika fainali iliyochezwa Wembley na kuisaidia timu yake kuwa mabingwa wa michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment