Wednesday, June 1, 2011

PUYOL KUFANYIWA UPASUAJI WA GOTI.

BARCELONA, Hispania
NAHODHA na beki wa klabu bingwa nchini Hispania pamoja na barani Ulaya FC Barcelona Carles Puyol kesho anatarajia kufanyiwa upasuaji wa goti.

Puyol (33) atafanyiwa upasuaji huo na madaktari wawili Ricard Pruna pamoja na Ramon Cugat huku ikiaminiwa kwamba atarejea katika hali yake ya kawaida kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

Kufuatia hatua hiyo Puyol amelazimika kuachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania ambacho kinajiandaa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Marekani pamoja na Venezuela mapema mwezi ujao.

Pia imeelezawa kwamba matatizo hayo ya goti yalichangia kutokujumuishwa kwenye kikosi kilichoanza mchezo wa hatua ya fainali ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Man utd waliokubali kibano cha mabao matatu kwa moja, na badala yake alipatiwa nafasi katika dakika za mwishoni za mchezo huo baada ya kutolewa kwa Daniel Alves.

No comments:

Post a Comment