Wednesday, June 15, 2011

UNITED YAMNYAKUA JONES.

LONDON, Uingereza
MABINGWA wa soka nchini Uingereza Manchester united wamekamilisha usajili wa beki wa klabu ya Blackburn Rovers, Phil Jones, kwa ada ya uhamisho wa paund million 17.

United wamekamilisha utaratibu wa kumuhamisha kinda huyo mwenye umri wa miaka 21, sambamba na kumsainisha mkataba wa miaka mitano.

Jones amekiri kufurahishwa na hatua hiyo ambapo alisema ni nafasi ya kipekee katika maisha yake ambayo amekiri imejitokeza kama bahati, kwani siku nyingi alikua na ndoto za kuitumikia klabu ya United.

Hata hivyo alisema bado anatambua mchango wa klabu yake ya zamani wa Blackburn ambayo ndio imemtambulisha katika ulimwengu wa soka na daima ataendelea kuipenda na kuienzi katika maisha yake yote.

Jones pia alikua akiwaniwa na klabu ya Arsenal pamoja na Liverpool.

No comments:

Post a Comment