Thursday, July 28, 2011

AGUERO AKAMILISHA UHAMISHO WA KIHISTORIA MAN CITY.

MANCHESTER, England
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa toka Argentina Sergio Aguero atakuwa ndio mchezaji ghali zaidi katika historia ya klabu ya Manchester City.

Man City wamekubali kulipa paundi milioni 35 kiasi ambacho kitaongezeka kutoka klabu yake ya zamani Atletico Madrid na atapewa mkataba wa miaka mitano utaomuwezesha awe anakunja paundi 200,000 kwa wiki, kitita cha kumchukua moja kwa moja kinatarajiwa kufikia paundi milioni 85.

Aguero akisaini karatasi za mashabiki wa Man City waliojitokeza kumlaki.
Aguero (23) ambaye atakuwa akivaa jezi namba 16 akiwa na City alikwenda Manchester Jumatano asubuhi baada ya kukatisha mapumziko na familia yake huko kwao.

Alichukuliwa vipimo vya afya kwa muda wa masaa matatu kabla ya kukubali kuitumikia klabu hiyo inayotumia Uwanja wa Etihad ambapo alilakiwa na mamia ya mashabiki waliojitokeza kumkaribisha na kusaini vitabu vyao.

No comments:

Post a Comment