Monday, July 11, 2011

ARSENAL YAKAMILISHA USAJILI WA GERVINHO.

KUALA LUMPA, Malaysia
KLABU ya Arsenal tayari imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast aliyekuwa akichezea klabu Lille ya Ufaransa Gervihno.

Mchezaji huyo ambaye alifunga mabao 15 na kutoa pasi zilizozaa mabao 10 na kuisadia Lille kutwaa taji la kwanza katika kipindi cha miaka 57 msimu uliopita, ametua Emirates kwa ada ya paundi milioni 12 ingawa hata mkataba wake haujawekwa wazi.

Wenger alithibitisha habari hizo kuhusu Gervinho wakati timu yake ilipowasili Malaysia, bila kuwa na mashambuliaji wake huyo mpya katika ziara yao ya mashariki ya mbali kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

Wenger alisema kuwa mchezaji huyo alisaini mkataba baada ya kutoka katika likizo yake na tayari ameshafanyiwa vipimo vya afya Alhamisi na kuruhusiwa kwenda nyumbani kuweka mambo sawa na familia yake.

No comments:

Post a Comment