Sunday, September 5, 2010

BARCELONA WAJIPANGA KUMUONGEZEA MKATABA DANI ALVES.

KLABU ya Barcelona wanajipanga kumuongezea mkataba beki wa kimataifa wa Brazil Dani Alves.


Rekodi ya uhamisho ya Mbrazil huyo kutoka klabu Sevilla ya ada ya Euro milioni 34 mwaka 2008 haijavunjwa mpaka leo, na ameendelea kufuarahia mafanikio akiwa na klabu hiyo baada ya kushinda mataji mbalimbali ya ligi na Klabu Bingwa ya Ulaya 2009.

Mkataba wa mchezaji huyo unaisha 2012, lakini ameonyesha nia ya kubakia katika klabu hiyo, na wanategemea ya kumuongeza mkataba wa miaka mitatu au minne ambapo yuko tayari kuitumikia klabu hiyo kwa miaka hiyo.

Manchester City walionyesha nia kumtaka mchezaji huyo katika kipindi cha usajili ambapo Rais wa klabu hiyo ameamua mumuongeza haraka mkataba huyo ili kumpiga bao bilionea huyo wa City.

No comments:

Post a Comment