Sunday, September 5, 2010

SIJUTII RAFU NILIYOMCHEZEA XABI ALONSO-DE JONG.

NIGEL de Jong amesema hajutii kitendo chake cha kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Hispania Xabi Alonso katika fainali za Kombe la Dunia.


Kiungo huyo anayechezea klabu ya Manchester City alimpiga kiatu cha kifua katika mchezo uliochezwa Afrika Kusini na mwamuzi wa mchezo huo tokea kipindi hicho alikiri kwamba alistahili kumtoa mchezaji huyo nje kufuatia rafu hiyo.

Hata hivyo De Jong alikaririwa akisema "Sijutii kitendo hicho hata kidogo. sikukusudia kumchezea hivyo."

"Na baada ya Kombe la Dunia nimerudi City nikiwa mchezaji tofauti, na hivyo ndivyo ninavyojisikia" alimalizia De Jong.

No comments:

Post a Comment