NAHODHA wa zamani wa England, David Beckham, anatarajiwa kurejea uwanjani kuitumikia klabu yake LA Galaxy Septemba 11 katika mchezo wa ligi dhidi ya Columbus.
Kiungo huyo wa kimataifa (35), yupo nje ya uwanja akiuguza majeraha ya kifundo cha mguu aliyopata muda mfupi kabla ya kuanza fainali za Kombe la Dunia 2010 akiwa AC Milan alikopelekwa kwa mkono.
Awali, mchezaji huyo aliripotiwa kurejea uwanjani Oktoba Mosi. "Nakunja vidole vizuri, nina matumaini nitacheza mchezo dhidi ya Columbus. Nilikuwa nje ya uwanja hivyo nadhani nitacheza dakika 15 au 20," alisema Beckham.
Maumivu ya nyota huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid, kulizima ndoto zake za kucheza fainali za Kombe la Dunia mara nne. Kiungo huyo amecheza mechi 115 za kimataifa.
Mara ya mwisho Beckham alicheza mchezo wa mwisho Oktoba 2009, England iliposhinda mabao 3-0 katika mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Belarus.
Kocha wa England, alipata shutuma kali kutoka kwa mashabiki baada ya kumtaka Beckham astaafu soka ya kimataifa kwa madai ya umri mkubwa. Kiungo huyo alipinga kauli hiyo na alidai ana nguvu za kuitumikia timu ya taifa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment