MASHAMBULIAJI wa Manchester United Wayne Rooney ameanza mazoezi Jumatatu asubuhi hii kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Klabu Bingwa ya Ulaya dhidi ya mabingwa wa scottland Rangers utakaochezwa kesho.
Kocha wa United Sir Alex Ferguson alimuondoa Rooney katika kikosi kilichopambana na na Everton Jumamosi, akisema kuwa alitaka kumlinda dhidi ya mashabiki wanaoweza kumzomea kutokana na kashfa yake binafsi inayomkabili.
Rooney anatarajiwa kuanza katika kikosi hicho kesho wakati timu itakapojaribu kuondokana na jinamizi la Jumamosi ambapo walitoka sare ya mabao 3-3 katika mchezo wa ligi dhidi ya Everton.
No comments:
Post a Comment