Monday, September 13, 2010

MADRID WAMMEZEA MATE ROONEY.

WAKATI mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney akiomba vyombo vya habari kutokushabikia kashfa ya maisha yake binafsi inayomkabili, kuna tetesi zimezagaa kuwa Real Madrid wameamua kuanza kumnyemelea mchezaji ili kuongeza nguvu katika kikosi chao.


Mourinho anajulikana kwa kuwazimia nyota wa Uingereza lakini kocha wa United Sir Alex Ferguson anamatumaini kuwa Mourinho hatataka kumnyakua mchezaji huyo kumpeleka Santiago Bernabeu.

Tayari Mourinho ameshamwambia Ferguson kuwa asijali kwani kumleta Rooney Madrid haitawezekana.

Kuna taarifa iliyotolewa kwa Mourinho na Rais wa Real Madrid Florentino Perez kuwa atatenga kiasi cha Euro milioni 65 kwa ajili ya mchezaji huyo.

"Uhamisho wa Rooney unawezekana" kilisema chanzo hicho cha habari.

"Kulikuwa na utata kuhusu uhamisho wa David Beckham na Cristiano Ronaldo lakini mwisho wa siku wote walitua Bernabeu."

Rooney aliachwa katika kikosi cha United kilichokwenda kucheza na Everton Ferguson akijaribu kumlinda na mashabiki ambao pengine wangemzomea kutokana na kashfa inayomkabili.

Kama hali ikiendelea kuwa mbaya kwa mchezaji huyo, basi atakuwa hana budi bali kuondoka Old Trafford.

No comments:

Post a Comment