KLABU ya Inter Milan inatarajia kufungua mazungumzo kuhusu uhamisho wa mchezaji wa kimataifa wa Brazil Kaka ifikapo Novemba mwaka huu baada ya Rais wa Inter Massimo Moratti kukubali uhamisho huo.
Tetesi kutoka gazeti moja la Italia zilisema kuwa Moratti tayari ameshaongea na bodi ya wakurugenzi ya klabu hiyo Ijumaa ambapo alitaka kutoa ruksa ya kumfukuzia mchezahi huyo. Lakini kama watafikia makubaliano wanayotaka.
Inter inamhitaji mchezaji huyto kwa mkopo lakini kwa makubaliano ya kumnunua mchezaji huyo moja kwa moja baada ya msimu mmoja, kama walivyomchukua Zlatan Ibrahimovic.
Klabu hiyo pia itatakiwa kulipa pesa za mchezaji huyo Real Madrid kwa vipindi tofauti kutokana na muda watakaokubaliana.
Hatahivyo, Inter itamchukua mchezaji huyo kipindi ambacho atakuwa fiti kwa asilimia mia moja.
Wanafanya hivyo kwa kuogopa yasije kutokea yaliyopita wakati Madrid walipowalaumu AC Milan kwa kuwauzia mchezaji huyo ambaye alikuwa majeruhi.
No comments:
Post a Comment