MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona David Villa amesema kuwa ametulia katika klabu hiyo na anafurahia msukumo anaopata akichezea mabingwa hao.
"Msukumo ninaopata kuhusu matokeo huwa yananifurahisha," "timu nyingi huwa zinajaribu kutuiga sisi na hilo linatufanya kuringia kikosi chetu." alisema Villa katika mkutano na waandishi wa habari.
""Nimetulia na nafurahi kuwa kuwa hapa najiona mwenye bahati. Tayari nimeshajua na wachezaji wenzangu pamoja na malengo yetu, kitu ambacho kinanirahisishia mambo yangu."
"Kwa kifupi najivunia kuwa sehemu ya kizazi hiki cha wachezaji na hapa najisikia niko nyumbani kama mmoja wa familia,"
"Huwa tunapasiana mipira na kushambulia kwa staili ya kipekee. Kwa pamoja Barca na timu ya Taifa ya Hispania tunaweza kucheza na timu yoyote na kuonyesha uwezo wetu. Naamini muonekano wetu ni mfano wa kuigwa na nafurahia hilo."
Mchezaji huyo pia aliongelea kuhusu nahodha wa Arsenal Cesc Fabregas na anaamini kuwa atajiunga na klabu hiyo katika siku za mbeleni.
"Moyo wa Fabregas uko kwa Barca na katika kipindi kifupi au baadae ataiacha Arsenal na kujiunga na sisi," alimalizia Villa.
No comments:
Post a Comment