Monday, September 20, 2010

"TORRES NI MDANGANYIFU," - FERGUSON

KOCHA wa Manchester United Sir Alex Ferguson amemtuhumu mshambuliaji wa Liverpool Fernando Torres kwa kudanganya, akisema kuwa alikuza tukio akitaka John O'Shea atolewe nje.

Katika mchezo baina ya timu hizo ulipigwa katika Uwanja wa Old Trafford ulishuhdia mshambuliaji wa United Dimitar Berbatov akifanya tukio la kukumbukwa kwa kupachika wavuni mabao matatu peke yake (Hat-Trick) na kupelekea timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Lakini tukiachana na ushindi huo kuna tukio ambalo O'Shea alimuanguasha Torres tukio ambalo lilizaa adhabu ndogo ambayo ilipigwa na Steven Gerrard kushinda bao la pili katika mchezo huo.

"Nililitizama mara ya pili tukio lile na inabidi niseme kuwa Torres alidanganya," alisema Ferguson.
"Alilifanya tukio lile liwe kubwa kwa kutaka mchezaji wetu atolewe nje."

No comments:

Post a Comment