Monday, September 20, 2010

MESSI NJE WIKI MBILI.

MSHAMBULIAJI wa Barcelona Lionel Messi atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa siku kumi tano baada ya kuumia kifundo cha mguu wakati yimu yake ilipoibuka na ushindiwa mabao 2-1 nyumbani kwa timu ya Atletico Madrid.

Kocha wa Barca Pep Guardiola alihakikishiwa kwamba Muargentina huyo hakuvunjika kifundo hicho cha mguu baada ya kuchezewa vibaya na Tomas Ujfalusi lakini ripoti ya waandishi wa habari ilisema kuwa atakosa kuitumikia timu hiyo kwa muda wa wiki mbili au zaidi.

Barca walikuwa wanaongoza baada ya beki huyo wa kimataifa Czech alipanda kadi nyekundu ya moja kwa moja ingawa tayari alikuwa na kadi ya njano kwa kumkwatua Muargenitiana huyo.

Messi alitolewa kwa machela akionekana akiwa katika maumivu makali, lakini Guardiola alisema kuwa nyota wake huyo hakuwa amepata maumivu makubwa sana kama alivyokuwa akihofu hapo mwanzo.

"Tumefurahi kushinda mchezo huu lakini pia tuna majonzi kwa kuumia kwa Leo (Messi)," aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano.

No comments:

Post a Comment