MSHAMBULIAJI wa Chelsea Didier Drogba amesifu ushindi waliopata wa mabao 4-0 dhidi ya Blackpool na kuendeleza mwanzo mzuri toka walivyoanza ligi mwaka huu.
Pamoja na kutengeneza nafasi nafasi nyingi katika kipindi cha pili, na magoli yote yaliyofungwa katika kipindi cha kwanza na Salomon Kalou, Drogba na Florent Maluda lakini Drgba anaamini kuwa wangefunga magoli mengi zaidi.
"Ulikuwa mchezo mzuri nafikiri tulionyesha uwezo na tulijaribu kushinda magoli mengi kadri tulivyoweza na tukapata mabao manne kipindi cha kwanza nadhani kipindi cha pili tulipata nafasi saba lakini hatukuzitumia vizuri," alisema Drogba baada ya mchezo huo.
"Nafikiri kidogo hatukuwa makini kwa kutokushinda magoli mengine zaidi, kutokuwa sehemu muafaka wakati pasi inapokufikia na hichi ni kitu ambapo inabidi tukifanyie kazi hata kama tulipata ushindi mnono.
Kukosekana kwa nahodha John Terry na msaidizi wake Frank Lampard kufuatia kuwa majeruhi majukumu ya kuiongoza timu hiyo alikabidhiwa Drogba ambapo alisema kuwa ni heshima kubwa kwake lakini alikuwa akiwaombea wachezaji wenzake hao kupata nafuu mapema.
"Najisikia furaha, nimekuwa hapa kipindi cha miaka sita. Lakini imekuwa ni vizuri kuwa pamoja nao. Nahitaji warudi uwanjani haraka lakini ni heshima kubwa kwangu kuwa nahodha wa kikosi hiki leo," alimalizia Drogba.
No comments:
Post a Comment