KABLA ya mchezo wao wa Jumanne wa Kombe la Ligi dhidi ya Tottenham, kocha wa Arsenal Arsenal Wenger amesema kuwa mashabiki wa klabu hiyo wasimlaumu William Gallas kwa kujiunga na mahasimu wao hao wanaotoka Kaskazini mwa London.
"Naamini kuwa majukumu yake ni kujitolea kwa nguvu zote katika klabu ambayo unachezea na alifanya hivyo alivyokuwa nasi." alisema Wenger.
"Unaweza kuwaelewa watu kutofurahia kama hujafanya hivyo lakini huwezi kuwaliza watu kama huna mkataba ulisainiwa na klabu na hicho ndicho kitu muhimu."
Wakati timu hiyo ikikabiliwa na mchezo huo dhidi ya Spurs, Wenger anatarajia kutumia nafasi hiyo kuwachezesha makinda wake ili wapate uzoefu.
Kipa Lukasz Fabianski, Johan Djourou, Emmanuel Eboue, Kieran Gibbs na mshambuliaji wa Mexico Carlos Vela ambao walikuwa benchi wakati wa mchezo dhidi ya Sunderland wataanza katika kikosi hicho, lakini hiyo pia itakuwa ni nafasi kwa wachezaji chipukizi Jay Emmanuel-Thomas, Bekin Afobe, Chuks Aneke na Henri Lansbury.
No comments:
Post a Comment