Tuesday, September 21, 2010

"NAJISIKIA KAMA NIMEFIKA MWEZINI HAPA MADRID." MOURINHO

KOCHA wa Real Madrid Jose Mourinho ametamba kwamba anajisikia furaha katika klabu hiyo akilinganisha kama kufika mwezini.

Akiongea Jumatatu kuhusu mchezo wao ujao dhidi ya timu ya Espanyol katika Uwanja wa Bernabeu, Mourinho alifafanua kuwa hawachukulii kiwango cha timu hiyo kirahisi na pia alionyesha jinsi gani anavyojivunia kufundisha mabingwa hao wa ulaya mara tisa.

"Espanyol ni timu yenye vipaji na inacheza soka la kuvutia," "watakuja hapa kushinda kama timu nyingine. hatuongozi ligi, lakini tunakaribia kufikia pale." alisema Mourinho kwenye tovuti ya klabu hiyo.

"Kuna timu nyingi ambazo ziko chini yetu na chache zilizotupita. Hivyo tunahitaji kuendelea kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri."

Kocha huyo Mreno aliendelea kusema kuwa kufundisha klabu hiyo ni sawa na kutua mwezini.
"Kwa jinsi ninavyijisikia, kuwa kocha wa Madrid ni sawa na kufika mwezini. Ni moja ya muhimu zaidi duniani.

"Hiyo inamaanisha nimejifunga hapa, lakini bado hatujashinda chochote. Tutaangalia kama tunaweza kuweka historia.

"Miaka kumi imepita haraka sana. Sasa nina furaha kama nilivyokuwa naanza kazi hii, na sidhani kama kuna kinaweza kubadilika katika miaka kumi ijayo.

"Natarajia kuwa kama Ferguson (Kocha wa Manchester United). Nitakuwa na miaka 70 lakini nitakuwa na morali wa kufundisha kama nilivyo sasa."

Mourinho alimalizia kwa kuonyesha kumwamini nyota wake Cristiano Ronaldo.

"Huwa anafanya kazi kubwa kila siku wakati wa mazoezi na awapo uwanjani. Huwa anasaidiana vizuri na wachezaji wenzake. Ni mchezaji bora." alimalizia Mourinho.

No comments:

Post a Comment