Tuesday, September 21, 2010

GHANA 'THE BLACK STARS' KUPEWA TUZO.

TIMU ya Ghana ambayo ilifika hatua ya robo fainali katika Kombe la Dunia lilifanyika Afrika Kusini mwaka huu wanatarajiwa kutunukiwa tuzo katika shrehe zinazotarajiwa kufanyika mwezi ujao London, Uingereza.

Timu inakuwa ni timu ya tatu kwa Afrika kufikia hatua hiyo katika historia ya Kombe la Dunia, lakini walitolewa kwa matuta na timu ya Uruguay.

Walijizolea wapenzi wengi wakiwa huko kutokana na jinsi walivyocheza kwa kujitolea na morali walionyesha, na kuzipita timu kama Uingereza, Ufaransa na Italia ambazo hazikufanya vizuri katika mashindano hayo.

Sasa timu hiyo ambayo imeshawahi kuwa mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika watajipanga kupokea tuzo yao hiyo kutokana na mafanikio waliyopata inayoitwa [Ghana UK Based Achievement (GUBA) awards] inayotarajiwa kufanyika London on October 24 mwaka huu.

Mojawapo watakaohudhuria hafla hiyo ni pamoja na nahodha wa timu hiyo John Mensah, ambaye anacheza kwa mkopo katika klabu ya Sunderland akitokea klabu ya Lyon, na Asamoah Gyan ambaye amejiunga katika klabu hiyo na alifunga magoli matatu katika michuano hiyo.

Mchezaji wa Fulham John Painstil na Michael Essien wa Chelsea ambaye alikosa michuano hiyo kutokana na majeruhi yanayokuwa yakimkabili nao watahudhuria tuzo hizo.

'Hii ni habari nzuri inatufanya kama timu kuona kuwa tunathaminiwa kitu tulicholifanyia taifa letu, si mara nyingi tunapata tuzo Ghana." alisema Mensah

'Ni heshima kubwa kuona ni jinsi gani tuzo za GUBA zitakavyotutia moyo.

Mtangazaji wa luninga wa huko Ghana Denta Sumpa ambaye pia ni mmoja wa wandaaji wa tuzo hiyo alisema timu hiyo inastahili tuzo hiyo kwa kuiweka nchi hiyo katika ramani ya dunia kwani katika michuano hiyo haikushangiliwa na waafrika pekee bali dunia nzima.

No comments:

Post a Comment