TAJI pekee alilobakiza Ricardo Carvalho akiwa na klabu ya Chelsea ni taji la Klabu Bingwa ya Ulaya. Beki huyo wa kushoto mwenye miaka 32 ameondoka katika klabu hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka sita, na kwa kuhama kwake amekwenda kukutana tena na Jose Mourinho ambaye alimpeleka Chelsea mwaka 2004.
Lakini wakati Ligi Kuu ya Hispania ikitajwa kuwa ligi bora duniani, ikiwa na wachezaji nyota wa dunia kama Leonel Messi na Cristiano Ronaldo, Carvalho alisema ligi hiyo ni tofauti na ya Uingereza.
"Wakati nilipokwenda Chelsea nilipata wakati mgumu tofauti na nilivyokuja hapa. Nimekulia Ureno na soka huko halina tofauti na hapa. nafikiri ni vigumu kucheza Ligi Kuu ya Uingereza. Wachezaji wa Uingereza wana nguvu zaidi kwa maana hiyo ni ngumu kucheza Chelsea kuliko hapa Madrid. Na kucheza huko kumenikomaza kama mchezaji. Nilikuwa na furaha katika kipindi chote cha miaka sita niliyochezea klabu hiyo." alisema Carvalho.
No comments:
Post a Comment