LOME, TOGO
SHIRIKISHO la Soka la Togo limemtuhumu kocha wa zamani wa timu hiyo Tchanile Bana kuwa amehusika katika sakata la kupeleka kikosi cha uongo kucheza na Bahrain na wamemfungia kwa muda wa miaka mitatu.
Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, shirikisho hilo lilisema kuwa maandalizi ya timu na usimamizi wa mchezo huo vyete vilipangwa na Tchanile Bana.
Timu ilitengenezwa na wachezaji ambao hawajulikani na kupokea kipigo cha mabao 3-0 mchezo ulichezwa Septemba 7 mwaka huu.
Bana, ambaye alikuwa kocha wa Togo katika miaka ya 2000 na 2004, tayari alishafungiwa miaka miwili kwa kupeleka timu Misri bila ya ridhaa.
Mjumbe wa Kamati ya Nidhamu ya shirikisho hilo alisema uchunguzi zaidi unafanyika kuhusu tukio hilo ambapo kuna viongozi wengine wanaweza kuchukuliwa hatua.
"Tukio zima lililotokea Bahrain lazima lichunguzwe kwa kina ili kuwanasa walioshirikiana na Bana." alisema Ofisa huyo.
No comments:
Post a Comment