BEKI wa Atletico Madrid Tomas Ujfalusi amefungiwa kucheza mechi mbili kufuatia tukio lake la kumchezea vibaya nyota wa Barcelona Lionel Messi Jumapili iliyopita ambapo timu hiyo ilipoteza mchezo huo.
Beki wa huyo wa kimataifa wa Czech alifanya tukio hilo katika dakika za majeruhi na kupelekea kutolewa nje kwa kadi nyekundu na kumfanya Messi kuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili.
Waandishi wa habari wa Hispania walikadiria kuwa beki huyo anaweza kufungiwa mechi kumi na mbili lakini Kamati ya Mashindano waliliona tukio hilo halikuwa la kukusudia hivyo kuamua atatumikia adhabu ya mechi mbili kama kawaida.
Ujfalusi ambaye tayari alishamuomba msamaha Messi kupitia ujumbe mfupi kwenye simu ya mchezaji mwenzake Kun Aguero atakosa michezo miwili wakati timu yake itakapopambana na valencia na Zaragoza.
No comments:
Post a Comment