MCHEZAJI Thierry Henry atakosa mchezo muhimu utaokaochezwa Ijumaa wakati timu yake ya New York Red Bulls itakapomenyana na timu anayocheza David Beckham ya Los Angeles Galaxy kufuatia kuumia mguu wake wa kulia.
Msemaji wa klabu hiyo alisema Jumanne kuwa mshambuliaji wa Ufaransa alifanyiwa vipimo kuangalia ni kiasi gani aliumia katika mchezo uliochezwa Septemba 4 dhidi ya Real Salt Lake ambao walipoteza.
Alicheza akiwa majeruhi wiki iliyopita na alitozwa faini ya dola 2,000 kwa kushangilia kwa kupiga mpira shuti baada ya mchezaji mwenzake Mehdi Ballouchy kufunga bao shuti hilo lilipelekea mpira mpira kumpiga golikipa wa Dallas Kevin Hartman na kumuumiza mguu.
"Tumeongea na Henry Jumatatu na tumeamua kwamba ni vizuri tukampumzisha kwa ajili ya afya yake," alisema Meneja wa Red Bulls Erik Soler. "Pamoja na mchezo unaotukabili Ijumaa, hatutaki kumuongezea maumivu zaidi ambayo amekuwa akicheza nayo karibu wiki mbili.
"Tunahitaji kuwa na uhakika kuhusu afya yake kwa ajili ya michezo yetu ya mwisho kwa kutarajia kuingia hatua ya mtoano, na kukaribia kutwaa kombe la (Major League Soccer [MLS]).
Mchezo wa Ijumaa utajumuisha wachezaji nyota wa ligi hiyo wakiwemo Landon Donovan wa Galax, Juan Pablo Angel na Rafael Marquez wote wa Red Bulls.
No comments:
Post a Comment