Sunday, September 12, 2010

WENGER ATAMBA KUCHUKUA KOMBE LA KLABU BINGWA MSIMU HUU.

KOCHA wa Arsenal Mfaransa Arsen Wenger anaamini kuwa timu yake iko fiti hivi sasa kunyakua kombe la Klabu Bingwa ya Ulaya msimu huu.


Arsenal haijawahi kushinda kikombe chochote cha Ulaya katika kipindi chote cha historia ya timu hiyo, wakati Wenger hajawahi kushinda mashindano akiwa na klabu yoyote barani Ulaya.

Mafanikio ambayo iliwahi kupata klabu hiyo ilikuwa ni mwaka 2006 ambapo walifika fainali lakini walipoteza mchezo huo kwa klabu ya Barcelona.

Wenger naamini katika safari yake hiyo ya kukisaka kikombe hicho cha Ulaya kikwazo kikubwa kitakuwa klabu ya Barcelona.

"Kama kuna timu ya kuogopa basi ni Barcelona," alikaririwa Wenger akisema.

"Hakuna timu isiyofungika lakini kuna timu za kufunga.

"Tuna malengo ya kushinda Klabu Bingwa, ndio. Tuna kikosi ambacho ni kizuri kikiwa na mchanganyika bora na uzoefu. Wakati ukiona timu yetu ikicheza, hutakuwa na swali kuhusu hilo." alimalizia Wenger.

Arsenal inaanza safari yake katika michuano hiyo msimu huu kwa kukutana na klabu ya Sporting Braga ya Ureno, Jumatano inayokuja.

No comments:

Post a Comment