KLABU ya Barcelona ndio klabu inyoongoza kwa mashabiki wengi Ulaya ikifuatiwa kwa mbali na klabu ya Real Madrid katika nafasi ya pili, wakati kuna klabu nne za Italia zinafuatia na klabu za Uingereza zikiwa mojawapo katika nafasi 20 za vilabu zenye washabiki wengi Ulaya kwa mujibu wa jarida moja michezo Ulaya.
Taarifa hiyo pia ilisema vigogo wa Ligi Kuu ya Uingereza Manchester United na Chelsea ndio zinazoongoza kwa mashabiki duniani lakini timu zimeshika nafasi ya tatu na ya nne mbele ya Bayern Munich ya Ujerumani.
Gazeti hilo ambalo hutoa tathmini ya vilabu 20 bora vyenye washabiki wengi utafiti wake ndani na nje katika nchi 17 za Ulaya (Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Italia, Hispania, Ureno, Uturuki, Uholanzi, Austria, Switzerland, Greece, Poland, Croatia, Bulgaria, Ukraine, Czech Republic na Russia).
Matokeo hayo yamepatikana baada ya kuwahoji mashabiki 10,200 wenye umri kati ya miaka 16 hadi 69 kutoka nchi mbalimbali zilizoorodheshwa hapo, kabla ya kuchapishwa.
Barcelona walipata asilimia 57.8 katika kura hizo wakati mahasimu wao Madrid walipata asilimia 31.3, Manchester United walikamata nafasi ya tatu kwa kuzoa asilimia 30.6. Chelsea, Arsenal na Liverpool walikamiliza listi hiyo kwa timu za Uingereza.
Italia imewakilishwa na timu nne katika listi hiyo ambapo AC Milan na Inter zipo katika nafasi ya saba na nane wakati Juventus ni ya kumi na Roma ya 19. Matokeo mengine ni kama yavyoonekana hapo chini na asilimia walizopata katika mabano.
Barcelona (57.8), Real Madrid (31.3), Manchester United (30.6), Chelsea (21.4), Bayern Munich (20.7), Arsenal (20.3), AC Milan (18.4), Inter (17.5), Liverpool (16.4), Juventus (13.1), Zenit St. Petersburg (12.6), CSKA Moscow (10.5), Spartak Moscow (9), Marseille (7.8), Ajax (7.1), Galatasaray (6.8), Lyon (6.6), Fenerbahce (6.1), Roma (6), Dynamo Kiev (5.3).
No comments:
Post a Comment