KIUNGO wa Barcelona Andres Iniesta amekiri kuwa timu yake ilikuwa na hofu kubwa wakati walipokubali kipigo cha mabao 2-0 wakiwa nyumbani Camp Nou dhidi ya timu ambayo imepanda daraja msimu huu ya Hercules.
Mabao mawili yaliyofungwa na mshambuliaji wa Paraguay Nelson Valdez yalitosha kuisaidia timu hiyo kuondoka na ushindi, ingawa barca walionekana kumiliki mchezo huo lakini hawakuweza mapigo.
Baada ya mchezo huo Iniesta alisema kuwa matokeo hayo yatawastua na kuwaamsha lakini wanatakiwa kuangalia mbele na sio kujilaumu kwa yaliyopita.
"Vikombe vyote tulivyoshinda kipindi cha nyuma haviwezi kutusaidia katika kipindi hichi. Ni matumaini yangu tutalifahamu hili na kuijindaa vyema kwa ajili ya mchezon ujao" alisema Iniesta
"Ni rahisi sana kuingiwa na woga, hakuna mtu ambaye anapenda kufungwa lakini tulijaribu na tulikuwa hatuna bahati tukifika golini kwao."
Barcelona watakuwa na nafasi ya kulipa kisasi katikati ya wiki wakati watakapocheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Panathinaikos, kabla ya kumenyana na Atletico Madrid.
No comments:
Post a Comment