RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Sepp Blatter pamoja na kupokea malalamiko kibao kuhusiana na baadhi ya matukio yaliyokea katika fainali za Kombe la Dunia lililofanyika Afrika Kusini, lakini Rais huyo amefurahishwa na jinsi alivyoziona fainali hizo, ingawa amekiri kuwa anafikiria kubadilisha baadhi ya sheria.
"Kwa ukweli niliona fainali nzuri za Kombe la Dunia mwaka huu. Mpira umekuwa mchezo wa mipango, huku timu zikienda pamoja. Kitu ambacho kinaweza kuwa na muonekano mzuri. kipindi cha nyuma kulikuwa na mipango rahisi ambapo timu hushambulia na kisha kuzuia." ilisema taarifa yake aliyotuma katika tovuti ya FIFA.
"Lakini kuna baadhi ya mechi katika hatua ya makundi katika michuano ya mwaka huu, ambapo tumeshuhudia baadhi ya timu zikizuia kufungwa kwa mchezo wa kutafuta suluhu. Suala hili nataka kulizungumza na Kamati ya Ufundi katika mkutano unaokuja."
"Tutajaribu kutafuta njia ambayo itawezesha kila timu kucheza kwa kujiachia katika mashindano kama haya, wakitafuta ushindi.
"Tunapanga kuchukua nafasi hiyo kuangalia kuhusu suala la muda wa ziada pia. Hivi sasa utaona timu nyingi zipaki mabasi katika kipindi chote cha muda wa nyongeza kuzuia mabao kwa njia yoyote. Kwa kuzuia hili, tunaweza tukaenda katika matuta moja kwa moja baada ya muda wa kawaida au kurudisha sheria ya bao la dhahabu (golden goal rule).
"Tutaangalia itakavyokuwa katika mkutano huo." alimalizia Blatter.
No comments:
Post a Comment