BARCELONA, Hispania.
KOCHA wa Real Madrid Jose Mourinho amekiri kuwa kikosi cha Barcelona kilikuwa bora baada ya kuifunga timu hiyo mabao 5-0 katika Uwanja Camp Nou.
Barcelona walitoka kifua mbele kwa mabao 2-0 wakati timu hizo zilipokwenda mapumziko na kuongeza mabao mengine katika kipindi cha pili na kjuihakikishia timu hiyo uongozi wa Ligi Kuu ya Hispania numa ya wapinzani wao Madrid.
"Timu moja ilicheza vizuri na nyingine vibaya," alikaririwa Mourinho akiwaambia waandishi wa habari baada ya mchezo huo. " Moja listahili kushinda na nyingine ilistahili kushindwa.
"Tumedhalilishwa? Hapana. Ni rahisi kukubali tulivyoshindwa, kwakuwa hatucheza vizuri."
Barcelona sasa wanaongoza ligi kwa pointi mbili mbele ya Madrid, ambapo mabao ya timu hiyo yalifungwa na Xavi na Pedro katika kipindi cha kwanza, David Villa alifunga mawili na la mwisho alimalizia Jeffren alieingia badala ya Xavi.
No comments:
Post a Comment