Wednesday, December 1, 2010

BECKHAM MGUU NJE MGUU NDANI EVERTON.

KIUNGO wa LA Galaxy David Beckham amesisitiza kuwa bado hajatoa uamuzi rasmi kuhusu yeye kucheza kwa mkopo katika klabu ya Everton.

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United alikuwa akicheza kwa mkopo katika klabu ya AC Milan katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ili kujiweka fiti na kumhakikishia kocha wa Uingereza Fabio Capello kuwa naweza kucheza katika kiwango cha juu.

Lakini kiungo huyo mwenye miaka 35, amekiri kuwa alishaamua toka nyuma kwamba hatarudi Italia kwa kipindi cha tatu, alipoumia na kusababisha aenguliwe katika kikosi cha Uingereza kilichokwenda katika Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment