ACCRA, Ghana
SHIRIKISHO la Soka la Ghana (GFA) limeteua majina matano ya makocha watakaowania nafasi ya kuinoa timu ya Taifa ya nchi hiyo 'Black Stars'
Ni kocha mmoja tu kati ya hao watano ambaye ni mzawa, Herbert Addo, ambaye ni kocha wa timu ya Taifa ya nchi hiyo kwa wachezaji wa ndani ambayo itacheza katika michuano ya CHAN iliyopangwa kufan yika Sudan mwaka 2011.
Wengine ni mchezaji wa kimataifa wa zamani ua Ufaransa Marcel Desailly, Mserbia Goran Stevanovic, Mreno Humberto Coelho na Can Vanli.
Kwa mujibu wa GFA, makocha hao watano watafanyiwa usaili baadae kabla jina moja kuteuliwa katikati ya mwezi Desemba.
No comments:
Post a Comment