ZURICH, Switzerland
SHIRIKISHO la Soka la Dunia (FIFA) imefikia uamuzi na kuwapa kibali Urusi kuwa wenyeji wa KOmbe la Dunia 2018. Urusi walikuwa wanakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka Uingereza, lakini Kamati ya Utendaji ya FIFA iliamua kuipa nafasi hiyo Urusi.
Kura zilipigwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo lenye wajumbe 24, na hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo kuandaa michuano hiyo mikubwa na muhimu duniani.
Wakati huohuo FIFA limeiteua nchi ya Qatar kuandaa fainali za Kombe la Dunia 2022. Katika kinyang'anyiro hicho Qatar ilikuwa ikikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa USA, lakini Kamati ya Utendaji iliamua kuipa nafasi hiyo Qatar.
Katika kinyang'aro hicho nchi zingine ambazo zilikuwa zikitaka nafsi hiyo ni pamoja na South Korea, Japan, Australia na USA, lakini zote hizo hazikufanikiwa.
Baada ya Kombe la Dunia 2002 liliandaliwa bara la Asia hii itakuwa ni mara ya pili kwa bara hilo kupata nafasi ya kuwa mwenyeji.
Ifuatayo chini ni orodha ya nchi ambazo zimeshawahi kuandaa michuano hiyo, washindi, idadi ya mabao pamoja na washindi wa pili.
No comments:
Post a Comment