Monday, December 6, 2010

KINYANG'ANYIRO CHA BALLON D'Or NI KATI YA MESSI, XAVI NA INIESTA.

PARIS, Ufaransa
WACHEZAJI wa Barcelona Andres Iniesta, Xavi Hernandez na Lionel Messi ndio majina ya wachezaji watatu waliteuliwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kugombea tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia maarufu kama "Ballon d'Or".

Viungo Iniesta na Xavi wameteuliwa kutokana na mchango wao mkubwa uliopelekea timu ya Taifa ya Hispania kunyakua Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza, wakati mshambuliaji Muagentina Messi yeye ametoa mchango mkubwa kwa timu yake ya Barcelona kuhakikisha inatetea taji lake la Ligi ya Hispania.

Messi alishinda mwaka uliopita wakati magazeti ya michezo ya Ufaransa walipotoa tuzo hiyo kwa mchezaji bora wa Ulaya. Wameungana mwaka huu na waandaaji wa tuzo ya mchezaji bora wa FIFA na kuunda tuzo moja.

Kocha wa zamani wa Inter Milan Jose Mourinho, Kocha wa timu ya Taifa ya Hispania Vicente del Bosque na Kocha wa Barcelona ndio majina matatu ya makocha walioteliwa kugombea tuzo ya kocha bora wa dunia kwa mwaka huu.

Mshindi atatangazwa January, 2011.

No comments:

Post a Comment