LONDON, England
KOCHA wa Arsenal Arsene Wenger amechukizwa na kauli aliyoitoa beki wa Manchester United Patrice Evra.
Timu hizo zikitarajiwa kukutana Jumatatu usiku katika Ligi Kuu ya Uingereza, Evra aliwatania wapinzania wao hao wakati akihojiwa na katika luninga moja ya Ufaransa akisema kuwa wakicheza na Arsenal ni kama sehemu ya mazoezi na kuongeza kuwa timu kukosa vikombe kwa kipindi kirefu kuwa ni ujinga.
Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa, Wenger alijitahidi kuzuia vita ya maneno na Mfaransa mwenzake huyo. Badala yake alifafanua kuwa timu yake haiwezi kubabaishwa na maneno ya kejeli ili kuongeza presha ya mchezo.
"Tunaongozwa na aina ya jinsi tunavyotaka kucheza mpira na sio kwa maneno ya mtu yoyote ambaye tunacheza naye. alisema Wenger. "Binafsi, naamini kwamba mchezaji mkubwa yoyote huwa anamuheshimu mpinzania wake na hicho ndicho tunachojaribu kufanya."
Arsenal ina rekodi nzuri ya michezo ya ugenini katika Ligi Kuu msimu huu na wanasafiri kwenda Old Traford kukutana na United ambao nao wana rekodi nzuri ya kushinda mechi za nyumbani.
No comments:
Post a Comment