Tuesday, November 9, 2010

BAGGIO ACHAGULIWA KUGOMBEA TUZO YA NOBEL.

MCHEZAJI mkongwe wa Italia Robert Baggio amechaguliwa kugombea tuzo ya amani ya Nobel.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 43 anajulikana kwa mchango wake katika kusaidia wasiojiweza duniani kote, wakati inayosimamia masuala hayo itakapotangaza aliyenyakua tuzo ya Amani shughuli ambayo inatarajiwa kufanyika Hiroshima, Japan.

Mchezaji huyo wa zamani wa Juventus na timu ya Taifa ya Italia alisaidia kuchangisha pesa kwa ajili ya Hospitali, waathirika wa tetemeko la ardhi na magonjwa yanayosumbua duniani.

Baggio ni mmoja kati ya wachezaji wengi ambao wanaendelea kutoa misaada kwa wanaohitaji duniani wakitumia umaarufu wao katika soka kuzindua kampeni na kuchangisha pesa kwaajili ya kusaidia.

No comments:

Post a Comment