Tuesday, November 9, 2010

SQUILLACI: HATUWEZI KUPOTEZA MCHEZO MWINGINE TENA.

Mchezaji wa Arsenal Squillaci akiwa hewani akipiga mpira kichwa huku mchezaji wa Shakhtar akimwangalia wakati timu hizo zilipocheza wiki iliyopita Arsenal ilifungwa 2-1.

LONDON, England
Mchezaji wa Arsenal Sebastian Squillaci ametoa onyo kuwa kama wakifungwa katika mchezo wao Jumatano dhidi ya Wolves itakuwa imetia doa timu hiyo katika kulifukuzia taji la Ligi Kuu msimu huu.

Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliyasema hayo kufuatia timu yake kupoteza michezo miwili wiki iliyopita dhidi ya Shakhtar Donetsk na Newcastle. Na anaamini kwamba timu hiyo haiwezi kupoteza pointi huko Molineux.

Alisema: "Bado tupo nafasi ya tatu katika ligi na tunaongoza katika kundi letu katika Ligi ya Mabingwa. Lakini kama unacheza katika timu kama Arsenal, baada ya kufungwa mechi kama mbili unahitaji kujirudi. Timu bora haiwezi kukubali kupokea vipigo vitatu mfululizo.

"Kwahiyo mchezo ujao utakuwa muhimu sana, tunahitaji kuonyesha kwamba Arsenal ni timu bora. Tunahitaji kujirekebisha vizuri katika mchezo wa Jumatano dhidi ya Wolves.

Kufungwa na Newcastle Jumapili ilikuwa ni mbaya kwa Arsenal, pamoja na Chelsea kupoteza mchezo dhidi Liverpool Anfield baadaye jioni.

"Yalikuwa ni matokeo ya kuaibisha kwasababu tulikuwa tumepata nafsi ya kuwasogelea Chelsea na Manchester United na kuongeza gepu kwa timu zilizopo nyuma yetu.

"Hatukua na sababu ya kufungwa. Wachezaji wengi hawakucheza dhidi ya Shakhtar. Tunahitaji kuzungumzia mahala ambapo tulikosea katika dhidi ya Newcastle na kupafanyia kazi.

No comments:

Post a Comment