Wednesday, November 24, 2010

BRAGA WASHEHEREKEA KUIFUNGA ARSENAL.

KOCHA wa timu ya soka ya Braga Domingos Paciencia amefurahishwa na timu hiyo baada ya kutoka kifua mbele dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Champions League baada ya kushinda mabao 2-0.

Paciencia alishuhudia timu yake ikihangaika kipindi cha kwanza, lakini walijirekebisha na kucheza vizuri kipindi cha pili.

"Niolihisi kama wanashindwa kukaa na mpira katika kipindi cha kwanza," alisema kocha huyo akiuambia mtandao wa UEFA.com. "Tulijua kwamba sio rahisi kucheza na timu kama Arsenal, kwani walikuwa wanataka kumiliki mchezo na tulijitahidi kutafuta nafasi wakati tulipomiliki sisi, ulikuwa mchezo mgumu.

"Mambo yote yalibadilika kipindi cha pili. Timu yangu ilicheza kwa kutulia, walisahau woga wao na kuongeza mashambulizi, kitu ambacho tulikimudu vizuri. Hiyo ndio siri ya ushindi wetu.

Wote sisi pamoja na mashabiki wetu tulistahili ushindi huu. Niloikuwa nategemea usiku huu utakuwa tofauti na nyingine na ilikuwa hivyo kweli.

"Tutaona nini kinaendelea sasa. Chochote kinaweza kutokea. Tunajua kwamba tulianza vibaya, dhidi ya Arsenal na hapa dhidi ya Shakhtar, lakini ni vizuri kuwaonyesha ubora wetu usiku huu." aliongeza Paciencia.

No comments:

Post a Comment