LONDON, England
KAMARI aliyocheza Kocha wa Arsenal Arsene Wenger kwa kumchezesha nahodha wake Cesc Fabrigas jana usiku ilimrudia baada ya mchezaji huyo baada ya mchezaji huyo kutolewa nje baada ya kujitonesha msuli wa nyuma ya paja katika mchezo ambao timu hiyo ilifungwa mabao 2-0 na Braga.
Mchezaji anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu, na atakosa michezo ya Ligi Kuu wakati timu yake itakapocheza na Aston Villa, Fulham na Manchester United Desemba 13.
Arsenal pia itamkosa mchezaji wake Emmanuel Eboue ambaye ameumia kifundo cha mguu baada ya kukwatuliwa kwa nyuma na Matheus ambaye alifunga mabao yote mawili ya Braga.
"Nimesikitika sana kwasababu nilisita kumchezesha," alikiri Wenger.
"Nilicheza kamari na imenirudia. inaonekana ni kama msuli wa nyuma ya paja kwa hiyo anaweza kuwa nje kwa wiki mbili au tatu."
Wenger aliwabwatukia wachezaji wa Braga kwa mchezo mbaya waliokuwa wakicheza na mwamuzi wa mchezo huo Viktor Kassai kutoka Hungary kwa kumpa kadi ya njano mchezaji Carlos Vela kwa kujiangusha wakati alitakiwa kutoa penati.
Wenger pia alichukizwa na bao la kwanza Braga lilivyopatikana wakati Arsenal ikiwa na watu kumi baada ya Eboue kutolewa nje baada ya kuumia.
"Ni vigumu kuelewa kwanini hatukupata penati," alisema.
Waamuzi watano sio suluhisho la tatizo.
"Tulifungwa wakati Eboue akiwa ameumizwa baada ya kuchezewa vibaya kitndo ambacho hakichukuliwa hatua yoyote na mwamuzi.
""Sehemu ya kurudi mchezoni ni ile penati bado sijaelewa jinsi Carlos Vela alipopewa kadi ya njano. imebakia kuwa kitu kisichoeleweka.
'Mwamuzi alifanya maamuzi ya ajabu usiku huu. Tulicheza na timu ambayo hawakutaka kucheza badala walikuwa wakitumia mipira mirefu ya kushtukiza (counter attack).
"Walifanya kila waliloweza ili kupooza mchezo."
Ingawa Wenger alikiri kuwa timu yake haikutengeneza nafasi nzuri, alidai pia kipigo walichopata dhidi ya Tottenham hakiwaathiri.
No comments:
Post a Comment