Tuesday, November 2, 2010

"LIGI YA MABINGWA ULAYA NI BORA KULIKO KOMBE LA DUNIA," - FERGUSON.

LONDON, England
KOCHA wa Manchester United Sir Alex Ferguson anaamini kuwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ni mizuri kuliko ilivyokuwa fainali za Kombe la Dunia lilifanyika mwaka huu Afrika Kusini.

Pamoja na michuano hiyo kuhudhuriwa na mashabiki wachache tofauti na msimu uliopita Ferguson haamini kuwa michuano hiyo imepoteza msisimko wake tofauti na Kombe la Dunia mwaka huu, ambalo alilifananisha na kitu cha kufurahia ili kupoteza muda.

"Umeshaona michuano sita ya Kombe la Dunia lililopita? ni bora ukaenda kwa daktari wa meno nadhani," alisema Ferguson akiwaambia waandishi wa habari.

"Ni kitu cha kawaida. Ikiwa umeona timu nzuri katika Kombe la Ulaya sasa na ukafikiria Ligi Kuu, Huwezi kupata mashabiki wengi Arsenal ikicheza na timu ndogo katika ligi au huwezi kupata presha na vituko kama ukiangalia Arsenal ikicheza na Manchester United.

"Ni sawa na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Inter ikicheza na timu ndogo haiwezi kupata mashabiki wengi."

Mscotland huyo amekiri kuwa mechi za mwanzo katika ligi hiyo hazikuwa na msisimko kama itakavyokuwa katika hatua zinazofuata, lakini akang'ang'ania kuwa michuano hiyo ni bora kimataifa.

No comments:

Post a Comment