Tuesday, November 2, 2010

FABRIGAS ASHINDWA KUIKABILI SHAKHTAR DONETSK.

LONDON, England
KOCHA wa Arsenal Arsene Wenger ameweka wazi kuwa kiungo wake tegemeo Cesc Fabrigas hatacheza mchezo wa Jumatano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Shakhtar Donetsk kutokana na maumivu ya nyonga.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania alikumbwa na hali katika mchezo dhidi ya West Ham ulichezwa mwishoni mwa wiki iliyopita lakini alimalizia mchezo huo ambao tulishuhudia Arsenal ikipata bao dakika za mwisho lilifungwa na Alex Song.

Ingawa, timu hiyo ina rekodi nzuri ya kushinda mechi zote tatu za michuano hiyo katika kundi H walilopo, Wenger amemuacha nyumbani Fabrigas, na aliongea na waandishi wa habari asubuhi hii ambap alisisitiza kuwa amepima uwezekana na ameona kwamba kiungo huyo atakuwa tayari kwa ajili ya mechi ya Newcastle mwishoni mwa wiki ijayo.

Alisema, "Ni mchanganyiko wa tahadhari na maumivu yanayomkabili. Ni hatari sana na hatuwezi kucheza kamari kwa hilo. Nafikiri ana nafasi nzuri kucheza Jumapili lakini kesho usiku itakuwa hatari sana.

"Hatuwezi kucheza kamari kwasababu alishaumia hapo kabla. ingawa sio tatizo kubwa, anahitaji kuwa fiti asilimia mia moja.

Wenger pia alisema kuwa Andrei Arshavin, Alex song na Denilson na wako katika hatari ya kutokucheza ingawa watasafiri na timu.

No comments:

Post a Comment